Posts

Umba sababu njema

UMBA SABABU NJEMA 12 Feb 2026 Mwalimu: Amani Ernest Kyamba SOGH team Let's do GOD'S work together. YESU alipokuwa anasulubiwa pale msalabani, shetani pamoja na wanadamu waliona wanamuua YESU. Kwamba ndo mwisho wa mwokozi, wakati huo YESU alikuwa anaumba sababu njema kuwa analitimiza andiko, na pia anamaliza kazi iliyomleta kwani alizaliwa ili afe kwa kusulubiwa kwa ajili yetu. Shetani aliyajua maandiko, ko labda naye angekuwa kipaumbele kuzuia YESU asisulubiwe lakini shetani ndo akasapoti kwani na yeye shetani yupo kwenye uwepo wa MUNGU, anafanya kazi ya MUNGU japo hapati thawabu kwa sababu ya makosa aliyoyafanya. Hata na sisi tukiwa tunafanya matendo ya uzima, kwa kujifariji kama sauli alivyojifariji kuwa heri ng'ombe na vinono visife kuliko kufa, Eti Bwana ana njaa ya sadaka. Sauli alihisi kuwa MUNGU ni masikini na anahitaji vitu vyake, kumbe MUNGU anahitaji utii wake. Tukiwa kama "sauli na shetani" basi tutafanya mambo yapasayo thawabu ila hatutapata th...

Je kwa nini namna ile?

M ​ ​Swali: hakukuwa na njia nyingine mbadala ya kutuokoa sisi mpaka YESU afe? ​Amani Ernest Kyamba SOGH Team. ​Let's do GOD'S work together. ​Njia zilikuwepo nyingi kwa sababu MUNGU ni mtendaji na muweza wa yote. Kwa hiyo MUNGU alitaka atumie njia ile ile ya wokozi sawasawa na njia ya uharibifu. Yaani alitaka/alipanga kumrudisha mwanadamu katika utakatifu sawasawa na njia ambayo mwanadamu aliingia katika upotevu. ​Adamu na Eva walipotea kwa kutokutii. YESU akaonyesha njia ya utii katika maisha yaliyozungukwa na kukosa utiifu, Luka 2:52, (akamtii MUNGU na wanadamu). Pamoja na kwamba mwanadamu hakutii na alizama dhambini yeye YESU akampa chaguo mwanadamu, la kukosa utii au kuamua kutii/kufanywa mtiifu. Kwani kupitia yeye mwanadamu akatambulishwa kwamba inawezekana kuwa mtii. ​Kutokutii kwa Adamu kulisababisha kifo. Kifo cha YESU kilimpa mwanadamu nafasi ya kumtii na kumtumikia MUNGU. Adamu alikula tunda akafa, YESU alikufa akaishi. Adamu alifukuzwa kwenye urithi wake, Y...

SOGH Team: nani unayemuangalia?

Tunajenga nia kwa ajili ya nani? SOGH Team Amani Ernest Kyamba. Let's do GOD'S work together. Note: Hili somo nimetumia reference ya cgm (christ gospel messenger) iliyopo kanisa la EAGT. Mimi nasali EAGT saza songwe kwa Daudi Before mbeyeye (true pastor). Hii haionyeshi mapungufu ya kanisani kwetu, ila nikaona nijifunze zaidi kupitia hali ambayo nadhani wengi wanaipitia kiroho na kimwili. #sisi tupo vizuri zaidi na tunapambana ili tuione mbingu pamoja na viongozi wetu wa kiroho (mchungaji na wazee wetu wa kanisa). Nimeona ni vyema nitumie mfano wa mazingira yangu ili hatimaye wote tuwe vizuri kabisa. Mara nyingi tunafanya mambo ya rohoni kwa kutumia reference fulani, yaani tuna copy. Jambo ambalo siyo. Tusiwape wanadamu wenzetu hali ya kwamba tunakopi kila kitu toka kwao kwa kuwa yale yalikuwa ni wakati ule (kwa mwanadamu) japo MUNGU ni yule yule. #kwa mfano nilisikia mfano kutoka kwa kaka kwamba CGM ya zamani ilikuwa moto tofauti na sasa. Ni sawa na ni kweli lak...

Ole

​05 Feb 2025 Ole kwetu sisi watumishi wa MUNGU ​nilikutana na watu wabaya wenye utisho porini na yote ni kwa kuwa kwanza nilipanda gari binafsi (nilijitenga na wenzangu waliokuwa kwenye basi mithali 18:1) na wakati huo nilikuwa na begi la thamani mno ambalo ni neno la MUNGU. ​Njiani porini nikashangaa begi limedondoka lenyewe kwanza kwa kuwa halikunistahili Mimi kushuka tu kumbe wale wa gari binafsi walikuwa dili moja na wale watu wa porini wanaotisha ambao walibeba visu, na vifaa vikali ili wanitishe.   ​Begi Lile sikuliona Wala chochote sikuliona nilipoteza neno ila ujuzi wa kupika sikupoteza basi shetani anahitaji ujuzi wangu wa kupika ko akaniambia nikapike chakula (junk) kinachoangamiza na kinachovutia. mimi nikajitambulisha kuwa Mimi ni mtumishi wa MUNGU wakasema kuwa hata wao Wana MUNGU wao, Mimi nikasema ni MUNGU wa mbinguni wakasema hata wao ni hivyohivyo..   ​Kumbe shetani anaweza akajigeuza kuwa malaika wa nuru ili kukupata wewe ambaye unajua neno la MUNGU...

Msingi imara(short notes)

​1. Kanisa na Msingi Imara ​ 07 Jun 2024 Kanisa na msingi imara. ​Hakuna nyumba inayojengwa pasipo msingi. uimara wa msingi ndio unaoamua uwezo wa nyumba kuhimili mabadiliko ya Hali ya hewa. ina maana kama kanisa linachezewa na shetani Ina maana kuwa kanisa halina msingi imara. makanisa mengi ya Sasa hayana msingi imara wa wokovu, yaani watu Wana sali lakini Wana hila mioyoni mwao, yaani kwaya zina ugomvi, na watu Wana maneno na hila wao kwa wao, watu wengini ni wasengenyaji uwepo wa dhambi katika kanisa unamuondoa MUNGU asiwepo kwenye kanisa Hilo na ndio maana ibada inapoa na watu wanabaki vile vile siku zote kwa Sababu mtu asiye na MUNGU anafananishwana jiwe ndani ya maji linalokaa kwenye maji ila haliruhusu maji kuingia ndani, yaani mwenye dhambi hawezi kumwona MUNGU hata siku Moja mpaka MUNGU atakapogeuza moyo wa mtu huyo uwe wa nyama. uwepo wa dhambi na kukosa utii wa neno la MUNGU kwa watu unaondoa uwepo wa MUNGU kwenye kanisa. ​ #yoshua 7:1. israeli ni mfano wa kanisa kam...

Mwamuzi(short notes)

​3. Nani amekufanya mwamuzi kwetu? ​ 20 Jan 2025 Nani amekufanya mwamuzi kwetu?//ijue thamani ya mwamuzi. Kutoka 2:14. ​Kwa Nini mwamuzi akati wamezoea utumwa.mwamuzi alikuja kwa lengo la kuonyesha Nia ya kuwasaidia lakini wao wanamshangaa na kumwona kama anajipendekeza. #MUNGU wa mbinguni amewavusha Israel kwenda nchi ya ahadi, lakini Wana wa Israel wanamshangaa Musa na MUNGU kwamba kwa Nini wamewatoa misri, kwa kuwa shida ya misri waliiona kuwa ni Raha. #na sisi utumwa wa dhambi tunauona ni Uhuru na uzuri kwetu. ​Mfano mwingine: 1 samweli 23:1-13. Daudi aliwaokoa keila kutoka katika mikono ya wafilisti, lakini keila walikuwa wanaenda kumsaliti Daudi kwa kuwa hawakutambua thamani ya mwamuzi. ​YESU Kristo ni mwamuzi!! Unaijua thamani yake?  Kuudharau wokovu ni dalili tosha kuwa. Harutambui thamani ya mwamuzi(YESU kristo) Tutapataje kupona tusipoujali wokovu mkuu namna hii. Wao waliijua thamani,kwa nini sisi tusiijue? Tunapaswa kuijua,ili tusije tukakataliwa japo tuliku...

Kuitambua neema(short notes)

​ 24 Sep 2024 Jinsi ya kuulinda utakatifu ​Utakatifu ni usafi kuanzia ndani (mawazo) mpaka nje. yaani mbegu ya mhindi haiwezi kuotesha maharage hivyo kama una mawazo ya kufisha ndani ya akili haijalishi unajizuiaje Bado hujashinda kwa kuwa utakatifu wa kweli unaanzia ndani. ​Unajua kwa Nini Wana wa Israel walishindwa kulifuata Sheria ni kwakuwa walitaka kuwa wazuri lakini chemichemi za mioyo yao zilitoa mambo maovu,, ikijaa chemichemi lazima maovu yatadhihirika na ndio maana tukiishi katika wokovu wa Sheria tunatoa maovu yaani tunaondoa maji ya chemichemi chafu ko yanaanza kujaaa Tena.. mda wote huo tutajiona watakatifu na wenye kumpendeza MUNGU lakini pale tu chemichemi ikijaa uovu unadhihirisha nguvu tukaanguka tena. ​ Warumi 7:15.. ​Je Nini tufanye ili tukamilike katika utakatifu? Ni kwa kufisha chemichemi chafu za asili ya Dunia hii za dhambi kwa kujitoa kikamilifu kwa MUNGU kupitia YESU Warumi 12:1.. kwa kuvuviwa (kuunda kiu ya kuacha dhambi) ambako ndiko kunamwita RO...